28 Julai 2025 - 19:46
Wizara ya Ujasusi ya Iran Yavunja Mtandao wa Kijasusi wa NATO na Mossad Katika Vita ya Kimya (Silent War / Covert War) ya Siku 12 + Video

Katika vita hii ya kimya kimya, vikosi vya kijasusi vya Iran vimepenya hadi kwenye ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Palestina inayokaliwa kimabavu) na kufanikisha kupata nyaraka nyeti sana za nyuklia, kijeshi na kiusalama kutoka kwa utawala wa Kizayuni, na kuvikabidhi kwa taasisi za Ulinzi za Taifa.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Wizara ya Ujasusi ya Iran imesema kuwa vita vya karibuni vya siku 12 dhidi ya Iran havikuwa tu mapigano ya kijeshi, bali vilikuwa ni mashambulizi ya pamoja na ya mseto kutoka kwa NATO ya kijasusi ya Magharibi, utawala wa Kizayuni na washirika wao, yaliyolenga kuangusha mfumo wa serikali, kusababisha vurugu na kuligawa taifa.

Kwa operesheni za kina za kushambulia na kujihami, wizara hiyo imefanikiwa kuwakamata mamia ya majasusi, magaidi na waharibifu, pamoja na kuzima njama nyingi za kigaidi na migogoro ya kiusalama.

Katika vita hii ya kimya (Silent War), vikosi vya kijasusi vya Iran vimepenya hadi kwenye ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Palestina inayokaliwa kimabavu) na kufanikisha kupata nyaraka nyeti sana za nyuklia, kijeshi na kiusalama kutoka kwa utawala wa Kizayuni, na kuvikabidhi kwa taasisi za Ulinzi za Taifa.

Ni Operesheni zipi zilizotekelezwa na Wizara ya Ujasusi?.

1_Kugundua na kuzima mipango 36 ya mauaji dhidi ya Viongozi wa Taifa.

2_Kuwakamata majasusi 20 waliokuwa wakifanya kazi na Mossad katika mikoa 13.

3_Kutumia nyaraka za siri za Israel kuboresha mashambulizi dhidi ya ardhi zinazokaliwa kimabavu za Palestina.

4_Kuweka pigo kwa majasusi na mitandao ya adui ndani ya Iran.

Hatua Gani Zilichukuliwa Dhidi ya Makundi ya Kigaidi?

1_Kukamatwa kwa makamanda 3 wa ISIS na magaidi 50.

2_Kutambuliwa kwa magaidi 300 wa kigeni kusini Mashariki mwa Iran.

3_Kuzimwa kwa mipango ya makundi ya kutaka kujitenga magharibi mwa Iran.

4_Kugunduliwa kwa maghala ya silaha za magaidi katika maeneo ya Kordestan ya Kaskazini mwa Iraq, Sistan, Kerman na Kordestan ya Iran.

5_Kuzima mradi wa kuanzisha “Serikali uhamishoni” na mpango wa mapinduzi uliokuwa ukiongozwa na Reza Pahlavi kwa msaada wa mawakala wa Kizayuni.

6_Kukamatwa kwa vibaraka 122 kabla ya kuanza kwa operesheni ya uasi mjini Tehran.

7_Kudhibiti malipo ya kidijitali yaliyokuwa yakipelekwa kwa vikundi vya waasi.

8_Kukamatwa kwa watu 98 waliokuwa na uhusiano na mtandao wa “Iran International”

Your Comment

You are replying to: .
captcha